Ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Afrika nchini
Uganda umetoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujitokeza kwa wingi na kutimiza haki
yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wawapendao.
Mkuu wa ujumbe huo wa AU, Sophia Okofor pia amewataka raia
wa Uganda kudumisha amani na kuwa watulivu baada ya uchaguzi. Bi. Okofor kutoka
Ghana aidha amewataka wanasiasa wanaowania nyadhifa mbalimbali kuheshimu
matokeo na kufuata mchakato wa kisheria endapo hawataridhishwa na matokeo ya
uchaguzi.
Uchaguzi wa bunge na rais umeanza asubuhi ya leo nchini
Uganda na tayari Rais Yoweri Museveni amepiga kura yake katika kituo cha
Rwakitura huku wagombea wengine wa nafasi ya urais pia wakipiga kura zao kwenye
vituo walikosajiliwa.
Wapigakura waliojiandikisha ni takriban milioni 15.3 na kuna
vituo 28, 010 kote nchini Uganda.
Wagombea urais ni wanane na kwa upande wa bunge, viti
vinavyowaniwa ni 290.
0 comments:
Post a Comment