Wapiga kura nchini Uganda
wanaendelea kupiga kura vituoni kuwachagua viongozi, ingawa katika
baadhi ya vituo upigaji kura ulichelewa kuanza.
Hili lilitokana na vifaa na karatasi za kupigia kura kutofikishwa vituo kwa wakati katika baadhi ya maeneo.Mjini Kampala, ambapo makao makuu ya Tume ya Uchaguzi yapo, bado kuna vituo ambavyo kufikia saa nne upigaji kura haukuwa umeanza.
Hata hivyo, tume hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, imeandika: "Tunabaki kuwa na matumaini na tunawahikishia kwamba nyote mtaweza kupiga kura leo. Tunasikitika kutokana na kuchelewa huku. Asanteni.”
Kuhusu iwapo
muda wa kupiga kura utaongezwa, tume hiyo kupitia mitandao ya kijamii
imesema kwa mujibu wa sheria, ni sharti vituo vifungwe saa kumi alasiri.
0 comments:
Post a Comment