Image
Image

Wapiga kura nchini uganda wajitokeza kupiga kura*Changamoto kadhaa za jitokeza,Picha 11 ziko hapa.



Wakati wananchi nchini Uganda waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wakiwa katika vituo vyao vya kupigia kura l;eo kumchagua Rais na wawakilishi wao wa Bunge dosari zimeanza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa vifaa vya kupigia kura na sehemu nyingine kuto kuanza zoezi hilo mapema.
Misururu mirefu ya wapiga kura imejitokeza kushiriki zoezi hilo licha ya kuwa na upinzani mkubwa na uchaguzi huo ukitajwa na wataalam wa mambo kuwa una hamasa kubwa mnoo nchini humo.
Inaelezwa kuwa,raia wapatao milioni 15 wa nchi hiyo waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanamchagua Rais mpya wa nchi hiyo pamoja na wawakilishi wao wa Bunge lijalo.
Wagombea wanane wanachuana kuwani kiti cha Rais hata hivyo kati ya wagombea hao wanane ni watatu tu miongoni mwao ndio waliotajwa sana katika kampeni za uchaguzi huo.
Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani nchini Uganda tangu mwaka 1986 anachuana na Kizza Besigye mgombea wa chama cha FDC na Amama Mbabazi aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wake. Uchaguzi wa leo unafanyika huku wapinzani wakiendelea kulalamika kwamba,serikali ya Rais Museveni imekuwa ikiwabana na kuwakandamiza wafuasi wao hasa katika kampeni za uchaguzi wa mara hii.
Huku Tume ya Uchaguzi ya Uganda ikisisitiza kwamba,uchaguzi wa leo utakuwa huru na wa haki,wagombea wa upinzani wameonya kuhusiana na hatua yoyote ile ya kuiba kura au kufanya udanganyifu.
Amama Mbabazi amesema, hatayakubali matokeo ya uchaguzi huo endapo itabainika kwamba,kulikuwa na mchezo mchafu wa kuiba kura. Weledi wa mambo wanasema, kuna uwezekano mkubwa Rais Museveni akashinda tea kiti cha urais na kuendelea kutawala nchi hiyo ya Afrika Mashariki.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment