Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi ya Ligi imemuelekeza
Katibu Mkuu wa TFF SELESTINE MWESIGWA kupeleka suala la tuhuma za kupanga
matokeo katika michezo miwili ya ligi daraja la kwanza baina ya KANEMBWA JKT
dhidi ya GEITA GOLD SC na POLISI TABORA dhidi ya JKT OLJORO kwenye Kamati ya
Nidhamu ya TFF kwa ajili ya uchunguzi na hatimaye kufanya uamuzi.
Kamati hiyo iliyokutana siku ya jumanne kuzungumzia suala
hilo imefikia maamuzi hayo baada ya kupitia taarifa za michezo hiyo na
vielelezo vingine na kupatwa na mashaka ya kuwepo kwa viashiria vya upangaji
matokeo.
Kutokana na suala hilo kuhusisha masuala ya kinidhamu na kwa
kuzingatia ibara ya 50 ya Katiba ya TFF na Ibara ya 69 ya Kanuni za
Nidhamu za TFF, Kamati hiyo ya Saa 72 ikaamua kulipeleka suala hilo
kwenye kamati husika ya nidhamu kwa ajili ya uchunguzi na hatimaye uamuzi.
Katika michezo hiyo JKT KANEMBWA ilifungwa mabao 8-0 na
GEITA GOLD SC katika mechi iliyofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma,
wakati POLISI TABORA ilishinda mabao 7-0 dhidi ya JKT OLJORO kwenye Uwanja wa
Ali Hassan Mwinyi mjini TABORA.
0 comments:
Post a Comment