Mkuu wa wilaya ya ARUSHA MJINI, FADHILI NKULU, amefunga kwa
muda machimbo ya migodi ya MORAM ya SEKEI na SHANGARAI yaliyopo katika kata ya
MOIVARO, wilayani humo, kufuatia migodi hiyo kuwa katika hali inayohatarisha
maisha ya watu
NKULU amechukua hatua hiyo baada ya kufanya ziara
katika maeneo mbalimbali yenye migodi ya MORAM ili kujionea namna shughuli hizo
zinavyofanywa na kubaini kuwa licha ya wachimbaji hao kuchimba kiholela,
machimbo hayo yapo kwenye hatari ya kuporomoka na kuhatarisha maisha yao.
Kutokana na hali hiyo, kamishna msaidizi wa madini kanda ya
kaskazini , ELIAS KAYANDABILA, na Meneja wa wakala wa barabara mkoa wa
ARUSHA, JOHNNY KALUKALE wamewaomba wachimbaji hao kutoa ushirikiano ili
waweze kusaidiwa kufanya uchimbaji katika hali ya usalama.
0 comments:
Post a Comment