Zaidi ya wananchi 4,700 wa Vijiji kumi katika wilaya ya
MBARALI mkoani MBEYA, wameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii, kuwalipa fidia
ili kupisha eneo la Hifadhi ya taifa ya RUAHA, ambayo wameamriwa kuhama tangu
mwaka 2007.
Wametoa maombi hayo wakimuomba Waziri mwenye dhamana ya
Maliasili na Utalii Profesa JUMANNE MAGHEMBE, kuingilia kati ili walipwe fidia
na kupisha hifadhi.
Kufuatia malalamiko hayo, Mkuu wa wilaya ya MBARALI, GULLAM
HUISSEIN KIFU amewaomba wananchi hao kuwa na subira wakati suala lao
linatafutiwa ufumbuzi.
0 comments:
Post a Comment