Image
Image

Uchaguzi wa Bunge la Iran ni azma na umoja wa kitaifa.


Kampeni za uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) zinaanza leo Alkhamisi kote hapa nchini.
Kwa mujibu wa kifungu nambari 56 cha sheria ya uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, kampeni za wagombea zinapaswa kuanza siku nane kabla ya zoezi hilo na kumalizika masaa 24 kabla ya kuanza upigaji kura. Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran, Muhammad Hussein Muqimi amesema kuwa, idadi ya watu waliopasishwa kugombea viti vya Bunge imefikia elfu 6 na 229.
Uchaguzi wa Bunge la kumi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ule wa Baraza la Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu utafanyika kwa wakati mmoja tarehe 26 mwezi huu wa Februari. Wizara ya Mambo ya Ndani inawajibika kutekeleza sheria na maafisa wote wanalazimika kutekeleza vyema na kikamilifu kanuni zote na kuchunga msingi wa kutopendelea upande wowote.
Wairani karibu milioni 55 wamekamilisha masharti ya kupiga kura. Kuhusu idadi ya masanduku ya kupigia kura yaliyokadiriwa kwa ajili ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Wizara ya Mambo ya Ndani amesema, inakadiriwa kuwa masanduku laki moja na 30 elfu yatatumika katika chaguzi hizo mbili.
Kushiriki idadi kubwa ya wananchi katika uchaguzi ni dhihirisho la uhalali na nguvu na sauti ya wananchi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na uchaguzi ujao una umuhimu mkubwa katika mtazamo wa kitaifa na kimataifa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, uhalali huo wa nguvu na sauti ya wananchi unapunguza mashinikizo ya kimataifa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Katika upande mwingine mahudhurio makubwa ya wananchi katika zoezi la uchaguzi hupandisha juu vigezo vya utaalamu na uzoefu wa wawakilishi wa Bunge na kutayarisha mazingira ya kupatikana Bunge lenye uwiano na chombo cha utekelezaji yaani Serikali. Vilevile idadi kubwa ya vyama vinavyoshiriki katika uchaguzi huo ni kielelezo cha demokrasia.
Inatarajiwa kuwa, mahudhurio ya wananchi wa Iran katika uchaguzi wa ujao wa Bunge na Baraza la Wataalamu yatakuwa makubwa zaidi ya chaguzi zilizopita na inahisika kwamba, wananchi mara hii wanataka Bunge la wataalamu na la watu wenye uzoefu. Kushiriki katika uchaguzi kuna maana ya kujali na kushughulishwa na mustakbali wa nchi. Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini karibu kila mwaka hufanyika uchaguzi mmoja wa kitaifa ndani ya Iran, suala linalopelekea kuwepo mabadiliko ya uongozi na viongozi wa sekta mbalimbali.
Mahudhurio makubwa ya wananchi wa Iran katika uchaguzi wa mwaka huu wa Bunge la Baraza la Wataalamu- kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma- yatawadhihirishia walimwengu nguvu na uwezo wa Iran ya Kiislamu na kuonesha tena kwamba, uchaguzi ni kielelezo cha azma na irada ya kitaifa ya kuonesha taswira ya umoja na mshikamano wa taifa la Iran ya Kiislamu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment