Rais Abd Rabbu Mansour Hadi wa Yemen, amemteua
kamanda mkuu msaidizi wa jeshi ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuutwaa tena mji wa
Sanaa kutoka kwa waasi. Rais Mansour amemteua Jenerali Ali Al Ahmar na
kumwapisha mjini Riyadh huku akiahidi kutwaa tena mji wa Sanaa.
Jenerali Al Ahmar aliasi jeshi la serikali na mwaka
2011 alijiunga na harakati za kumwondoa madarakani aliyekuwa rais wa Yemen Ali
Abdullah Saleh.
Maofisa walio karibu na Rais Hadi wanasema hatua
hiyo inalenga kutafuta uungaji mkono wa makabila yenye silaha yanayomtii
Jenerali Al Ahmar, dhidi ya waasi.
Waasi wanaoungwa mkono na Iran na wapiganaji
wanaomtii aliyekuwa Rais wa nchi Bw Saleh, walitwaa udhibiti wa mji wa Sanaa
mwezi Septemba mwaka 2014
0 comments:
Post a Comment