Ndege ndogo iliyowabeba watu 23 imetoweka ikiwa
maeneo yenye milima nchini magharibi mwa Nepal.
Ripoti zinasema mabaki ya ndege hiyo yamepatikana
ingawa hakuna habari kuhusu majeruhi au manusura.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Pokhara,
magharibi mwa mji mkuu Kathmandu, kwenda Jomsom, eneo ambalo watu wengi
wanaoenda kukwea milima ya Himalaya huanza safari yao ya kukwea milima hiyo.
Ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na maafisa wa
udhibiti wa safari za ndege wa Pokhara dakika 10 baada ya kupaa.
Hakuna viwanja vya ndege kati ya maeneo hayo mawili
na inahofiwa kwamba ndege hiyo imeanguka.
Maafisa wanasema ndege hiyo ya shirika la Tara
Airlines ilikuwa na marubani watatu na abiria 20, mmoja wao raia wa Uchina na
mwingine wa Kuwait. Wawili kati ya abiria waliokuwa wamebebwa na ndege hiyo
walikuwa watoto.
Ajali za ndege hutokea mara kwa mara nchini Nepal.
Tangu mwaka 1949, kumetokea zaidi ya ajali 70
zilizohusisha ndege za kawaida na helikopta, na vifo vya watu 700.
0 comments:
Post a Comment