Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
ameelezea matumaini yake kwamba viongozi duniani watajitolea kwenye mkutano wa
kilele kuhusu masuala ya kibinadamu utakaofanyika mwezi Mei huko Uturuki ili
kupunguza wakimbizi wa ndani duniani angalau kwa asilimia 50 ifikapo mwaka
2030.
Kauli hiyo ameitoa alipotembelea kambi ya wakimbizi
wa ndani ya Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kusisitiza
kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani inazidi kuwa kubwa na jumuiya ya kimataifa
inatakiwa kuboresha misaada ya kibinadamu. Idadi ya wakimbizi wote duniani ni
ndogo kuliko idadi ya wakimbizi wa ndani ambao hawajavuka mipaka kutafuta
makazi na usalama.
Hadi kufikia mwaka 2014, watu milioni 38
walilazimika kukimbia makazi nchini mwao kutokana na vurugu.
0 comments:
Post a Comment