Idadi ya watu waliofariki kufikia sasa katika janga
la kimbunga kilichopiga kisiwa cha Fiji Jumamosi iliyopita imepanda na kufikia
42.
Maafisa nchini humo wanahofu kuwa huenda idadi hiyo
ikapanda zaidi, kwani data za watu waliofariki zinatoka maeneo ya ndani zaidi
vijijini.
Nyaya ya nguvu za umeme iliyokuwa imekatizwa sasa
inaunganishwa huku vyumba vya kuhifadhia maiti vikiwa bado havina umeme.
Kwa sababu hiyo, serikali sasa imezishauri familia
zilizopoteza wapendwa wao, kuwazika au kuzichoma maiti haraka iwezekanavyo, kwa
sababu ya ukosefu wa vifaa vya kuhifadhi maiti.
0 comments:
Post a Comment