Kilabu ya Barcelona imefuzu asilimia 95 katika
michuano ya robo fainali ya kombe la vilabu bingwa barani Ulaya ,mkufunzi wa
Arsenal Arsene Wenger amesema baada ya kilabu yake kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi
ya mabingwa hao wa Uhispania.
Raia huyo wa Ufaransa aliilaumu safu yake ya
mashambulizi kwa kushindwa kufunga na kukosa kujua cha kufanya wakati wa mechi
hiyo.
Alex Oxlaide Chamberlain na Olivier Giroud walikosa
nafasi za wazi kwa upande wa Arsenal kabla ya Barcelona kufunga bao lao la
kwanza.
''Vile tulivyomaliza nafasi zetu ilikuwa
matatizo.Nilihisi katika kipindi cha mwisho tulikosa kiufanya kitu
muhimu,''alisema Wenger.
''Barcelona wamefuzu asilimia 95,lakini tunataka
kwenda huko kucheza.Hatutakwenda huko kuchezewa,''aliongezea.
0 comments:
Post a Comment