Image
Image

Kesi ya LEMBELI ya kupinga matokeo ya uchaguzi yahamishiwa mahakama ya wilaya ya Kahama.



Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi katika Jimbo la Kahama Mjini iliyofunguli wa na aliyekuwa mgombea ubunge  wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo  CHADEMA JAMES LEMBELI dhidi ya mgombea wa  Chama cha Mapinduzi, JUMANNE KISHIMBA imehamishiwa katika mahakama ya wilaya ya kahama na kuanza kusikilizwa rasmi .
Kesi hiyo inasikilizwa na  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu  MOSES MZUNA  katika mahakama hiyo ya wilaya   lengo likiwa ni kuwapa fursa wananchi wa jimbo hilo kusikiliza shauri ambalo linagusa maslahi yao.
Wakizungumza na  Radio One Stereo   baadhi ya wananchi waliokuwa wamefika mahakamani kusikiliza shauri hilo wame sema  kitendo cha mahakama kuu kuhamishia kesi katika mahakama ya wilaya hiyo kimetoa fursa kwa wananchi wengi kusikiliza mwenendo wa shauri linalowagisa moja kwa moja.
Kabla kesi ya msingi kutajwa na kuanza kusikilizwa Wakili wa JUMANNE KISHIMBA  ambaye ni mlalamikiwa    ameieleza mahakama kuwa upande wa mlalamikaji umeshindwa kukamilisha vipengele vilivyokuwa vinahitajika mahakamani ili kukamilisha ushahidi .
Baada ya Jaji MOSES MZUNA kusikiliza hoja za kila upande amei ahirisha kesi  hiyo  hadi tarehe 29 mwezi huu .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment