Maafisa wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani wamesema
wameona ushahidi kuwa serikali ya Rwanda imekua ikichangia matukio ya machafuko
katika nchi jirani ya Burundi.
Inaelezwa kuwa Rwanda imekuwa ikiwapa silaha na mafunzo
wakimbizi waliokimbia machafuko nchini Burundi.
Burundi imetumbukia mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe tangu
Rais Pierre Nkurunziza alipoamua kugombea uraisi kwa muhula wa tatu.
Maafisa hao wa Marekani wanasema taarifa walizo nazo kutoka
kwa maafisa wenzano waliopo kwenye kambi za wakimbizi nchini Rwanda, zinasema
Rwanda imekuwa ikihusika na vurugu katika nchi jirani ya Burundi.
Akihojiwa na Bunge la Congress mmoja wa wanadiplomasia
amesema kuna taarifa za kuaminika kwamba wakimbizi wa Burundi ikiwa ni pamoja
na watoto wamekuwa wakipewa mafunzo katika makambi nchini Rwanda, na kufunzwa
kupambana kwa silaha na serikali.
Image copyright Getty Ghasia zilizuka nchini Burundi mwaka
jana baada ya rais wa nchi hiyo kusema atagombea kwa muhula wa tatu.
Serikali za nchi hizi mbili zina makabila ambayo ni
mahasimu, na kuna ongezeko la wasiwasi wa kimataifa kuwa mgogoro mwingine wa
kikabila inaweza kuota mizizi katika eneo hilo.
Tayari Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda amekanusha tuhuma
hizo ambapo amesema Umoja wa Mataifa unapaswa kutafuta mikakati ya kutatua
mgogoro ya kisiasa badala ya kutafuta nani wa kumtupia lawama.
0 comments:
Post a Comment