Madai ya unyanyasaji wa kingono nchini Iran katika kituo
kimoja cha runinga yamesababisha wanawake nchini Iran kuvunja ukimya wao na
kuanza kulijadili swala hilo kwa kina ambalo kwa utamaduni wao ni mwiko.
Sheena Shirani,msomaji habari katika runinga ya Press TV
ambayo hutumia lugha ya kiingereza ,alivunja mwiko huo kwa kuzungumza
unyanyasaji wa kingono aliokumbana nao mbele ya wasimamizi 2 wa kituo hicho kwa
kipindi kirefu.
Madai yake yalisambazwa hadharani wakati alipochapisha
mtandaoni mazungumzo ya simu ambayo mtu anayedaiwa kuwa msimamizi wake kazini
Hamid Reza Emadi mara kadhaa alitaka kulala naye.
Kufuatia kisa hicho Shirani aliwacha kazi na kuondoka katika
taifa hilo na baadaye kuchapisha rekodi hiyo ya sauti ambayo imesikizwa zaidi
ya mara 120,000 katika ukurasa wake wa mtandao wa facebook na mtandao mmoja wa
habari uliopo nje ya taifa hilo.
Vilevile alichapisha majibizano yake ya maandishi na Emadi ambapo
anamtaka kuondoa sauti hiyo katika mtandao wake.
0 comments:
Post a Comment