Idadi ya watu kumi na mmoja wamefariki dunia na ishirini na
sita wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la Simba mtoto lililokuwa
likitokea jijini Tanga kuelekea Dar es Salaam kupata ajali kwa kugongana na
lori lilokuwa limebeba mchanga katika kijiji cha Pangamlima eneo la Segera
wilayani Muheza mkoani Tanga
Mpasa sasa maiti zipatazo sita zimeshatambuliwa na ndugu na
jamaa zao huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali teule ya
wilaya ya Muheza.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Mihayo Msikela
amesema kwamba chanzo cha hiyo ni dereva wa lori kuendesha gari huku akiwa
amesinzia huku akiwa akiwa kwenye mteremko huku akiwa katita njia ambayo sio
yake na hivyo kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo na majeruhi.
Aidha katika upande mwingine kwa waliofariki dunia ambao
wametambuliwa na ndugu zao ni pamoja na Mama mkwe wa Mwandishi wa habari wa
Mlimani TV khamis Dam Mbaya pamoja na mke na mtoto wake.
Kwa mujibu wa ndugu na marafiki wa karibu wa Khamisi Dam
Mbaya nikwamba waliofariki katika familia watazikwa huko mkoani Tanga kutokana
na kuharibika vibaya.
Waliofariki dunia katika familia hiyo wanaelezwa huenda
wakazikwa hivi leo,lakini juhudi za kumpata Khamis Dam Mbaya zinaendelea licha
yakuwa katika wakati mgumu.
Mwenyezi Mungu awape wepesi katika kipindi hiki kigumu.
0 comments:
Post a Comment