Waziri wa Kilimo,Uvuvi na Ufugaji Mwigulu Nchemba amefanya
ziara ya kushtukiza katika machinjio ya ukonga mazizini na kubaini madudu
makubwa usiku wa kuamkia hivi leo.
Katika ziara hiyo ya Waziri Nchemba imebaini madudu hayo
ikiwamo kukamata ng”ombe 200 wakiwa wanaingizwa kwenye machinjio bila kibali
halali.
Katika ukamataji huo wa Ng”ombe waziri Nchemba amebaini kuwa
Ng”ombe 20 tu kati ya 200 ndio walio na kibali cha kuchinjwa pekee, huku ushuru
wa ng”ombe 180 umekwenda mifukoni mwawatumishi waovu na wenyelengo ovu na baya
dhidi ya serikali.
Kwa hatua hiyo sasa Waziri Nchemba amewasimamisha kazi mkuu
wa mnada wa pugu ambaye siku si nyingi aliaminiwa na serikali na kupewa
jukumu aongoze mnada huo pamoja na watumishi wote waliotajwa kwenye ubadhilifu
huo.
Waziri wa Kilimo,Uvuvi na Ufugaji Mwigulu Nchemba ameviagiza
sasa vyombo vya dola kuwakamata watumishi hao mara moja na kufikishwa
mahakamani huku hatua zingine za kiofisi akiahidi kuanza muda si mrefu.
Aidha Nchemba amewashukuru wa Halmashauri ya Ilala na Mbunge
wa Ukonga Mh.Mwita Mwikwabe (CHADEMA) na vyombo vyote kwa ushirikiano waliouonesha
kwake hadi kubaini madudu hayo.
0 comments:
Post a Comment