Serikali imewasilisha bungeni mapendekezo ya mpango
wa maendeleo wa taifa 2016/7 na muongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya
serikali kwa mwaka 2016/7 ambapo imebainisha vipaumbele vyake vitano ikiwemo
sekta ya viwanda huku ikitegemea kutumia zaidi ya shilingi tirilioni 22 kwa
ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo.
Mpango huo umewasilishwa na waziri wa fedha na
uchumi Mh Dk Philip Mipango ambapo amesema sekta ya viwanda itapewa msisitizo
mkubwa zaidi.
Wakichangia mpango huo baadhi ya wabunge wamesema
umekuwa mzuri japo yapo baadhia ya maeneo ambyo inaonekana serikali iliyasahau
na hivyo kuna haja ya kuuboresha zaidi ili uweze kuwa na tija.
Kwa upande mwingine baaadhi yao wamesema watendaji
wa serikali wanapaswa kuongeza kasi ili mipango iliyobainishwa iweze
kutekelezwa lakini kama haitakuwa na hivyo ni dhahiri kuwa mpango huo
hautalisaidia taifa.
Awali bungeni hapo kabla ya kuwasilishwa kwa hoja
hiyo na Mh waziri wa fedha kulitokea mvutano wa kikanuni na hatimaye kanuni
zikatenguliwa na bunge likakaa kama kamati ili kuweza kuijadili hoja hiyo.
0 comments:
Post a Comment