Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa imewahukumu
kwenda jela miaka mitatu wahamiaji 83 raia wa Ethiopia walioingia nchini bila
kibali huku pia ikiwahukumu jela miaka mitano dereva na utingo wa lori
waliowasafirisha wahamiaji hao kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea nchini
Malawi.
Akisoma hukumu hiyo mahakamani hapo hakimu mkazi wa
mahakama ya hakimu mkazi ya mkoa wa Iringa Mheshimiwa Edrew Scout amesema
mahakama imezingatia maombi yote ya wahusika lakini kwakuwa biashara ya
usafirishaji binaadam imezidi kushamili nchini mahakama imeona ni vema
watuhumiwa hao wakatumikia adhabu ya kufungwa jela miaka mitatu au faini ya
shilingi milioni moja na kurejeshwa kwao baada ya adhabu.
Mahakama hiyo imewakuta na hatia dereva na utingo wa
lori lililowasafirisha wahamiaji hao Hance Mwakyoma na Alex Adam kwenda jela
miaka mitano au faini ya shilingi milioni moja na nusu ambapo dereva wa lori
Bwana Hance Mwakyoma amelipa faini hiyo na kuachiwa huru.
Katika kesi nyingine ya wahamiaji 12 raia wa
Ethiopia waliokamatwa hivi karibuni wakiwa kwenye gari ya kusafirisha magazeti
ya kampuni hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu makazi ya mkoa wa Iringa Richard
Kasele amewahukumu kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya shilingi laki
tano watuhumiwa hao huku kesi ya dereva wa gari lililowasafirisha pamoja na wasaidizi
wake wawili ikiahirishwa hadi tarehe 15 mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment