Serikali inaandaa mkakati kutafuta mitaji kutoka
taasisi za fedha ili kuuwezesha mfuko wa zao la kahawa nchini kuweza kutoa
huduma zilizokusudiwa kwa wakulima.
Mkakati huo wa serikali unaelezwa na Naibu waziri wa
kilimo mifigo na uvuvi Mhe.William Ole Nasha bungeni mjini dodoma wakati
akijibu swali la mbunge wa mbozi Mhe.Paschal Haonga aliyetaka kujua ni lini
serikali itaweka ruzuku kwenye pembejeo za kilimo kama vile mbolea ili
kuwapunguzia wakulima gharama za uzalishaji.
Naibu waziri Ole Nasha amesema hivi sasa mfuko huo
unakabiliwa na changamoto ya kukosa mitaji ya kutosha kutoa huduma zote
zilizokusudiwa kutokana na michango ya wadau kuwa midogo ikilinganishwa na
mahitaji.
Aidha mhe Ole Nasha amesema serikali imeendelea
kutoa ruzuku ya madawa na mbegu bora kwenye mazao ya pamba na korosho na kwa
upande wa mazao ya chai na kahawa ruzuku imekuwa ikitolewa kwenye miche bora
ili kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao hayo.
0 comments:
Post a Comment