Serikali imewataka wananchi wanaopata huduma
mbalimbali za afya ya mama na mtoto katika hosipitali,vituo vya afya na
zahanati za umma kutumia masanduku ya maoni kutoa malalamiko yao pale wanapoona
hawajatendewa haki na watoa huduma ili hatua dhidi yao zichukuliwe na kukomesha
ukiukwaji wowote wa haki za mteja.
Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee
na watoto Mhe. Hamis Kigwangala ametoa wito huo kwa wananchi wakati akijibu
swali lililoulizwa na mbunge wa viti maalum Faida Mohamed Bakar aliyehoji
kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa huduma na haki za afya ya uzaji katika maeneo
mbalimbali nchini na kuhatarisha maisha ya wanawake.
Naibu waziri Kigwangwala amesema katika
kutekeleza suala hilo serikali itaweka na kusimamia masanduku ya maoni katika
sehemu zote za kutolea huduma za afya ili wananachi wapate fursa ya kutoa maoni
yao kwa mtoa huduma yetote atakayekiuka haki za mteja na kuchukuliwa hatua.
Mhe.Kigwangwala ameongeza kwa kuesema kuwa mazoezi
ya ukaguzi na ufuatiliaji wa kushtukiza yanayofanywa na kiongozi yeyote wa
serikalini mwenye dhamana ya kusimamia huduma za jami katika vituo vya kutolea
huduma za afya vya umma na binafsi tayari yameanza kuzaa matunda kwenye
uboreshaji wa huduma na haki kwa wateja kwenye sekta hiyo
0 comments:
Post a Comment