Shambulizi linalokisiwa kuendeshwa na wanamgambo wa
Taliban katika chuo kimoja kaskazini magharibi mwa Pakistan limesababisha vifo
vya karibu watu 20 na kuwajeruhi wengine 50.
Karibu saa tatu tangu kuanza kwa shambulizi hilo
afisa mmoja wa kijeshi alisema kuwa ufytuaji wa risasi umekwisha lakini
wanajeshi walikuwa wakiendesha msako katika chuo cha Bacha Khan kilicho eno la
Charsadda.
Jeshi lilisema kuwa washambuliaji wanne waliuawa
huku Taliban wakisema kwa washambuliaji wanne wa kujitoa mhaga walihusika
kwenye shambulizi hilo.
Taliban waliwaua wanafunzi 130 kwenye shule moja
katika mji ulio karibu wa Peshawar mwaka 2014.
Msemaji wa Taliban aliliambia shirika la habari la
AFP kuwa shambulizi hilo ni la kulipiza kisasi oparesheni ya kijeshi dhidi ya
ngome za Taliban.
Siku chache zilizopita baadhi ya shule katika mji wa
Peshawar zilifungwa kufuatia ripoti kuwa wanamgambo walikuwa wakipanga
mashambulizi.
0 comments:
Post a Comment