Serikali imeitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania (TPA) kuongeza makusanyo yake kwa mwaka kutoka sh. Bilioni 600 ambazo
walijipangia mpaka kufikia Trilioni 1 ili fedha zisaidie kutatua matatizo ya
wananchi, kuliko kuacha zikipotea kwa uzembe.
Akizungumza mkoani Mtwara baada ya kufanya ziara
katika Bandari ya mkoani humo, Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Mhe.
Makame Mbarawa, amesema serikali ya awamu ya Tano imejikita katika kuhimiza
uwajibikaji kwa watendaji, na haitokuwa na huruma kwa mtu yeyote atakayefanya
kinyume na hayo.
Amesema, bandarini kuna udhaifu mkubwa ambao
serikali haiwezi kuuvumilia na kwamba itaendelea kuchukua hatua mpaka pale
itakapojiridhisha kuwa pamekaa vizuri hata ikibidi kubakiza wafanyakazi
wachache kuliko kuwa nao wengi ambao hawaleti tija inayohitajika.
Kwa upande wake, meneja wa Bandari ya Mtwara,
Prosper Kimaro, amesema miongoni mwa mipango waliojiwekea ni kuongeza Gati 4
katika Bandari hiyo ambapo kwa kuanzia wataanza kwa ujenzi wa Gati moja ambayo
tayari mamlaka imeshaamua na ujenzi wake utatumia fedha za ndani.
0 comments:
Post a Comment