Naibu waziri mkuu wa Syria na waziri wa mambo ya nje Bw.
Walid Muallem amesema, serikali ya Syria imeahidi kushiriki kwenye mazungumzo
baina ya Wasyria bila masharti. Pia amesisitiza kuwa "ni watu wa Syria tu
ndio wanaoweza kuamua mustakabali wa nchi yao".
Wakati huohuo, Wizara ya ulinzi ya Russia imekanusha shutuma
zilizotolewa na Uturuki kuhusu vikosi vya anga vya Russia kushambulia hospitali
nchini Syria na kusema lengo cha kitendo hicho cha Uturuki cha kuipaka matope
Russia kupitia vyombo vya habari ni kwa ajili ya kung'ang'ania udhibiti wake katika
sehemu za kaskazini na kaskazini magharibi za Syria. Na msemaji wa wizara ya
ulinzi ya Russia Bw. Igor Konashenkov amesema, makundi ya kigaidi nchini Syria
bado yanapata msaada kupitia mpaka kati ya Uturuki na Syria, na baadhi ya nchi
zinatarajia kulinda njia hiyo isiharibiwe.
0 comments:
Post a Comment