Serikali imekiri kuwepo kwa upungufu wa vitendea
kazi katika Idara ya usalama nchini hali inayoifanya idara hivyo kutofanya kazi
zake kwa ufanisi.
Katika kuimarisha hali ya usalama serikali imesema
kuwa itahakikisha inaboresha na kulipatia jeshi la Polisi nyenzo za kutosha ili
liweze kukabiliana na tatizo la ukosefu wa usalama nchini.
Ni katika kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao
cha bunge asubuhi ya leo, ambapo baadhi ya wabunge wanaitaka serikali kuweka
wazi mipango iliyo nayo katika kuboresha utendaji kazi wa jeshi la polisi
nchini.
Kuibuka kwa makundi yanayoharamishwa ya ‘Mazombi’ na
‘Masoksi’ yanayoripotiwa kuwahangaisha wakaazi wa Unguja, kunaendelea
kuwapa hofu wakaazi visiwani humo,
Baadhi ya wabunge wamejitokeza kudai kuwepo kwa
upungufu mkubwa wa vitendea kazi vya kuiwezesha idara ya polisi nchini
kutekeleza majukumu yake
Wakati huo huo serikali imesema inaendeleza miradi
mbalimbali ya kuboresha idara hiyo ikiwemo ujenzi wa nyumba 35000 za polisi,
kuanzisha miradi ya kuwapa mikopo polisi pamoja na nyongeza ya mishahara kwa
watumishi hao.
0 comments:
Post a Comment