Juhudi za kutafuta miili na mali zilizozama katika
kivuko cha MV KILOMBERO II kilichozama tarehe 27 mwezi uliopita zinaendelea
ambapo gari moja limeibuliwa kutoka katika kivuko hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero LEPHY GEMBE
amesema gari iliyoibuliwa ni mali ya idara ya misitu huku juhudi
zikiendelea kuitafuta gari la benki ya CRDB.
GEMBE amesema boti za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania –JWTZ pamoja na Wizara ya Maliasili zinaendelea kutoa huduma za
kuvusha watu bure.
Juhudi za kuibua kivuko hicho zinaendelea ili kuweza
kufanya uchunguzi wa kugundua chanzo cha ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment