Wakazi wa mkoa wa Morogoro wamesisitiza Serikali
kurudisha utaratibu wa kuonesha moja kwa moja matangazo yote ya Vikao vya Bunge
ili waweze kuona wanachofanya wawakilishi wao waliowapa Dhamana ya
kuwawakilisha Bungeni.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini
Morogoro Wananchi hao wamesema hawakubaliani na utaratibu wa serikali wa kuamua
TBC kurusha moja kwa moja sehemu ya Maswali na majibu na baada ya hapo
kurekodiwa na kurushwa usiku.
Wamebainisha kuwa pamoja na stesheni zingine za
televisheni ikiwepo Star tv kurusha matangazo hayo,lakini wananchi wana
haki ya kuangalia televisheni yao ya taifa kwa kuwa inaendeshwa kwa
kodi za watanzania .
Uamuzi wa serikali wa kusitisha matangazo ya
moja kwa moja bungeni baada tu ya kipindi cha maswali na majibu kumendelea
kuleta simtofahamu kwa wanachi walio wengi , ambapo mkoani, Morogoro uamuzi huo
umepokelewa kwa hisia tofauti.
Wakazi wa mkoani hapo wanaona kufanya hivyo ni
kutaka kuwakosesha haki ya msingi ya kupata habari kwa
kuona nini wanacho kifanya wawakilishi wao waliowatuma .
Serikali ilitoa mapendekezo hayo ikidai
kupunguza Gharama zinazo tumika kurusha matangazo hayo ambapo zaidi ya
Bilion 4 hutumika kwa mwaka, huku ikielezakuwa zaidi ya asilimia 80 ya
watanzania hawaangalii matangazo hayo muda wa mchana.
0 comments:
Post a Comment