Image
Image

Serikali yaridhishwa na kasi ya mradi wa Songosongo mkoani Lindi.



Serikali  imesema imeridhishwa na mradi wa gesi wa Songosongo ulioanza uzalishaji wake mwaka 2004 ambao unatarajiwa kukamilika ifikapo Februari 10 mwaka huu kwa visima 12 vya gesi kukamilika.
Akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa visima vya gesi wilayani Kilwa mkoani Lindi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa  amesema Serikali inaridhishwa na mwenendo wa uchimbaji wa visima vya gesi asilia unavyoendelea na anaamini itakuwa na faida kwa watanzania woteAmesema kuwa amefurahishwa na mwendendo wa ujenzi wa visima hivyo vya gesi ambapo amewataka waendesha mradi huo  Kampuni ya Pan African Energy wanaoendesha mradi huo wa uchimbaji wa visima vya gesi, kukamilisha haraka visima vilivyobaki
Kwa upande wake Meneja Operesheni wa Kampuni ya Pan African Energy ambao wanaendesha mradi huo wa uchimbaji wa visima vya gesi, Onestus Mujemula amesema hadi sasa wamekamilisha uchimbaji wa visima saba vinavyofanya kazi kati ya 12
Bofya HaPA---http://shamakala360.blogspot.com.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment