Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
WILLIAM LUKUVI amewataka wawekezaji wa kigeni waliopewa ardhi nchini kwa ajili
ya mifugo kutumia vizuri ardhi hiyo kwa kufuga kisasa badala ya kuchunga mifugo
kienyeji kama wanavyofanya wananchi wa kawaida.
Waziri LUKUVI ametoa agizo hilo baada ya
kutembelea shamba la mwekezaji la DARAKUTA lililopo katika kijiji cha
GIJAMEDA bonde la KIRU wilaya ya BABATI mkoani MANYARA.
Waziri LUKUVI amebaini kwamba mwekezaji huyo hafugi
kwa kisasa na badala yake anafuga mifugo kwa kuchunga jambo ambalo halizingatii
matumizi bora ya ardhi.
0 comments:
Post a Comment