Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha imetangaza kuanza
kuvifunga vituo vyote vya kulelea watoto ambavyo wamiliki wake wanatumia fursa
hiyo kujinufaisha.
MKUU wa Wilaya ya Arumeru Wilson Ngambaku
amesema Serikali inapitia usajili wa vituo hivyo pamoja na kuangalia
utendaji kazi wake na kwamba vituo vyote ambavyo vinafanyakazi kwa ajili ya
maslahi ya watu binafsi vitafutiwa usajili wake mara moja.
Nkambaku ametoa kauli hiyo wakati yeye pamoja na
wanachama wa Chama cha mapinduzi walipotembelea kituo kimoja cha yatima ikiwa
ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 39 ya CCM ambapo kwa mkoa wa Arusha
yamefanyika katika kata ya Ngarenanyuki Wilayani Arumeru
Katika maadhimisho hayo wanachama wa chama cha
mapinduzi Mkoani Arusha wametumia fursa hiyo kufanya shughuli mbalimbali za
kijamii ambapo Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Bernad Murunya amesema
ni vyema sasa wanachama kuondoa makundi na kuzidi kukijenga chama hicho ambacho
amekitaja kuwa mfano wa kuigwa ndani ya bara la Afrika
Shughuli nzote hizo zinaafanyika wakati huu ambapo
chama tawala cha mapinduzi CCM ambacho ni zao la vyama vya TANU na ASP
kinaadhimisha miaka 39 tangu kuzaliwa kwake.
0 comments:
Post a Comment