TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini, NEC, imetakiwa
kutolifanya suala la uchaguzi mkuu wa nchi kama jambo la dharura ili kuondoa
kasoro zinazo jitokeza kila kipindi cha uchaguzi mkuu kinapofika.
Kufanya hivyo kumetajwa kutasaidia kupunguza ama
kuondoa dosari za uchaguzi ikiwemo ya muda mdogo wa uandikishaji wapiga kura,
idadi kubwa ya wanaojiandikisha kutokupiga kura, ucheleweshaji wa vifaa vya
uchaguzi vituoni na ucheleweshaji wa matokeo.
Tahadahari hiyo imetolewa katika kipindi hiki ambapo
Nec imebaini kuwa mwaka 2015 watanzania Milioni 15,596,110 kati ya
22,658,247 waliojiandikisha sawa na asilimia 67 ndio waliopiga kura, huku kura
402,248 zikikataliwa baada ya kuharibika kutokana na wapigakura kukosa elimu
sahihi ya upigaji wa kura hasa vijijini.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala wa
NEC,Hamisi Mkunga, Mkoa wa Morogoro kupitia jimbo la Morogoro kusini Mashariki
ndilo lililo ongoza kwa uharibifu wa kura 28,961 , wakifuatiwa na jimbo la
Misungwi,, Dodoma mjini, Ubungo, Kinondoni na Ukonga ambako wapiga kura
waliweka alama za X ama V katika karatasi ya kura.
Hayo yamesemwa Katika kikao cha Tathmini ya Uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015 kilicho ishirikisha NEC na Asasi za Kiraia kutoka katika
mikoa ya Katavi, Rukwa na Mbeya ambaapo viongozi wa mkoa huu wamehimiza suala
la NEC kuzingatia wingi wa vituo na ukubwa wa majimbo wakati wa ugawaji wa
vifaa vya uchaguzi
Uchaguzi mkuu wa mwaka jana umemuweka madarakani Mh
Rais John Pombe Magufuli Makamu wa Rais Mh Samian Suluhu, Waheshimiwa Wabunge
na Madiwani.
0 comments:
Post a Comment