Washukiwa 7 wa ugaidi wameripotiwa kutiwa mbaroni na
polisi katika operesheni iliyotekelezwa kwenye miji mitatu nchini Uhispania.
Polisi waliarifu kutekeleza operesheni hiyo kwa
mafanikio katika miji ya Valencia na Alicante nchini Uhispania, na mji wa Ceuta
unaopakana na mipaka ya Afrika ya kaskazini.
Washukiwa hao wanaodaiwa kujihusisha na DAESH,
walitiwa mbaroni baada ya kuonekana wakisaidia makundi ya kigaidi yanayoendesha
shughuli zao nchini Iraq na Syria.
Polisi wametoa maelezo na kuarifu kwamba washukiwa 4
kati yao ni raia wa Uhispania wenye asili ya Jordan, Morocco na Syria.
0 comments:
Post a Comment