Miili askari polisi watatu waliofariki kwenye ajali
ya barabarani wakati wakioongoza msafara wa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli
mkoani Singida Jumamosi ya wiki hii, imeagwa na kusafirishwa kwenda kwao
mikoa ya Dar-Es-Salaam, Lindi na Kigoma tayari kwa ajili ya mazishi.
Hata hivyo kutokana na umati mkubwa wa watu
waliojitokeza na kuchelewa kuanza kwa shughuli hiyo hadi kufika saa 11 jioni
kabla ya kumalizika, waombolezaji hawakuruhusiwa kupita karibu ya majeneza ya
marehemu kwa ajili ya kutoa heshima zao mwisho kama ilivyozoeleka.
Majonzi, simanzi na huzuni vikiwa vimetawala
katika viwanja vya polisi Mjini Singida, wakati miili ya askari watatu
waliokufa kwenye ajali ikiwasili kwa dua na sala tayari kusafirishwa kwenda
kwao kwa ajili ya mazishi
Askari hao Inspekta Mwigelwa Miraji, Staff
Sajenti Elias Mrope na Sajent Gerald Ntondo walikufa kwenye ajali wakati
wakiongoza Msafara wa Rais aliyekuwa akirejea Dodoma kutokea Singida kwenye
sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi.
Viongozi mwaandamizi wa Polisi na Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dokta Pareseko Kone pamoja na salamu zao za pole na rambirambi kwa
ndugu, jamaa na marafiki amesema ajali hiyo ilitokana na gari lao kupasuka
gurudumu na hivyo kupelekea ajali hiyo
Ajali hiyo ya gari ya Polisi imetokea jumamosi
majira ya saa 9: 40 alasiri katika eneo la Isuna-Ikungi barabra kuu ya kuelekea
Dodoma na kusababisha vifo vya askari hao watatu na kujeruhi wengine wawili.
0 comments:
Post a Comment