Watu wanne wameripotiwa kufariki baada ya kutupiwa
bomu la kurusha kwa mkono katika kitongoi cha Kinama mjini Buumbura katika
usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na meya wa jiji
la Bujumbura Freddy Mbonimpa, mabomu matatu yalirusha katika kitongoji cha
Kinama na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo mtoto mdogo mwenye umri wa
miaka 12 aliekuwa akiuza mayai.
Watu wengine kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa ma
kupelekwa hospitali ili kupewa matibabu.
Mtaani Musaga kumeripotiwa pia kurushwa kwa guruneti
dhidi ya Polisi na kuwajeruhi watu wanane.
Hakuna kundi lolote limejinasibu kuhusika na
shambulio hilo.
0 comments:
Post a Comment