Wanamgambo wa kundi la Taliban wameripotiwa kuteka
nyara mabasi mawili yaliyokuwa yamebeba abiria 100 waliokuwa wakisafiri
kuelekea Kabul kutoka mkoa wa Faryab nchini Afghanistan.
Mkuu wa polisi mkoani Faryab Sayid Aaka Anderabi,
alitoa maelezo na kuarifu kwamba wanamgambo hao waliyasimamisha mabasi hayo ya
abiria katika mji wa Karamkol ulioko mkoani Mirzakum.
Mahali walikopelekwa abiria hao waliotekwa nyara bado
hakujajulikana.
Anderabi aliongezea kusema kwamba maafisa wa usalama
wameanzisha shughuli zao kwa ajili ya kuwaokoa abiria hao waliotekwa nyara.
Kundi la Taliban halijatoa maelezo yoyote kuhusiana
na tukio hilo.
Takriban miezi 6 iliyopita, kundi la Taliban pia
liliwahi kuteka nyara basi moja lililokuwa na abiria 12 katika mji wa Gazne
nchini Afghanistan.
0 comments:
Post a Comment