Image
Image

Wauaji wa Sheikh Shehatta wahukumiwa kifungo miaka 14 Misri .

Mahakama moja ya Misri imewahukumu kifungo cha miaka 14 jela watu kadhaa waliohusika na mauaji ya mwanazuoni wa madhehebu ya Shia wa nchi hiyo, Sheikh Hassan Shehatta.

Watu watatu wamepatikana na hatia ya kumuua mwanazuoni huyo wa Kishia na wenzake kadhaa baada ya nyumba yake kuvamiwa na mawahabi katika mkoa wa Giza.
Tarehe 24 Juni mwaka 2013 genge la watu waliongozwa na viongozi wa kisalafi katika kijiji cha Abu Muslim lilishambulia eneo lenye Waislamu wa madhehebu ya Shia na kuwaua watu wanne akiwemo Sheikh Shehatta na ndugu yake, Muhammad Shahatta. Shahidi Sheikh Hassan Shehatta alikuwa miongoni mwa viongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Misri na aliuawa shahidi kwa kupigwa mawe, marungu na kadhalika hadi kufa.
Sheikh Muhammad Jabir ambaye ni miongoni mwa viongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Misri ameiambia Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo kuwa, makundi ya kiwahabi yanawalenga raia hasa wafuasi wa Ahlul Bait (A.S) nchini humo na ametaka kuzidishwe ulinzi na kuwadhaminia usalama raia wote hususan wale wanaolengwa kwa sababu za kiitikadi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment