MTIKISIKO wa hali ya kisiasa Zanzibar umebisha hodi
katika Kanisa ambapo Jukwaa la Wakristo Tanzania limetoa onyo.
Viongozi wa wa Dini ya Kikristo kupitia Jukwaa la
Wakristo Tanzania kwenye taaifa waliyoitoa leo, wametuhumu Serikali ya Jamhuri
ya Muungano Tanzania kwa kushindwa kukabiliana na mkwamo wa kisiasa visiwani
humo.
Wamesema, udhaifu wa kikatiba uliovumiliwa kwa muda
mrefu bila kutatuliwa ndio chanzo kikuu cha sintofahamu visiwani humo na
kusababisha wananchi kuishi kwa mashaka.
Jukwaa hilo limefikia hatua hiyo wakati ambapo hali
ya kisiasa visiwani humo ikiendelea kuyumba kutokana na matukio yanayoonesha
kuanza kwa uvunjwaji wa maani.
“Sisi viogozi tunafadhaishwa na hali ya Zanzibar kwa
sasa. Hali ya Zanzibar isingefikia hapo iwapo serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ingechukua hatua ya kutatua mgogoro huu,” inaeleza sehemu ya
taarifa hiyo iliyosainiwa na Askofu Justice Ruwa’ichi.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba, upungufu uliopo kwenye
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio unaosababisha kushindikana
kutatuliwa kwa matatizo ya Zanzibar.
“Hata hivyo udhaifu huu wa katiba ya Muungano
hauondoi wajibu wa Serikali ya Muungano kuhakikisha haki na amani vinatawala
Zanzibar,” ameeleza kwenye taarifa hiyo.
Ameeleza, serikali na taasisi zinazosimamia suala la
uchaguzi wanapaswa kuhakikisha uhuru, haki na amani Zanzibar zinalindwa na
kuheshimiwa.
Pia wameshauri kwamba, “mchakato wa Katiba Mpya ya
wananchi (Rasimu iliyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba) urejeshwe ili
kuondoa utata wa serikali ya Jamhuri ya Muungano kushiriki masuala ya
Zanzibar.”
0 comments:
Post a Comment