ALOYCE Lukulu, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo Bonde la Mto Rufiji (Rubada), amepandishwa kizimbani jana kwenye
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za wizi wa Sh. 136 milioni
Akisomewa shitaka hilo na Denis Lekayokwenye, Wakili
wa Serikali mbele ya Warialwande Lema, Hakimu Mkazi Kisutu, la kuiba
fedha za mamlaka ya umma, ametuhumiwa kutenda kosa hilo mara tatu.
Mtuhumiwa anadaiwa kuiba Shilingi 50 milioni za
Rubada kati ya tarehe 1 hadi tarehe 10 Agosti 2010 kwa kutumia cheo chake.
Lukulu pia anadaiwa kuiba Shilingi 36 milioni
kati ya tarehe 1 hadi 30 Novemba mwaka 2010.
Anakabiliwa na kosa lingine la wizi wa fedha za umma
Shilingi 50 milioni kwenye mamlaka hiyo.
Mtuhumiwa huyo amerejeshwa rumande kwa kukosa
dhamana. Kesi hiyo itaendelea tena 24 Machi mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment