Makamu wa rais Mh.Samia Suhulu Hassan ameziagiza
halmashauri zote nchini kuhakikisha vituo vyote vya afya vyenye huduma za uzazi
vinawekewa huduma za dharura kwa wajawazito haraka iwezekanavyo mara baada ya
bajeti ya mwaka 2016/17 kutoka.
Mh.Samia amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa
ufunguzi wa siku ya utepe mweupe nchini yenye lengo la kuwakumbuka kina mama
wajawazito na waliopoteza maisha siku ya kujifungua ambapo licha ya kusikitika
juu ya ongezeko kubwa la vifo vya wajawazito na watoto wadogo amebaini
serikali haitafumbia macho swala hilo.
Mwakilishi wa waziri wa afya,maendeleo ya jamii
jinsia wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu,Profesa Mohamed Bakari amesema kila siku
wajawazito 24 wanaojifungua hufariki na wengine kupata vilema vya maisha na
kuwa tayari wizara yake imeshaanda mikakati mbalimbali ya kupunguza na
kutokomeza kabisa tatizo hilo.
Baadhi ya washiriki siku ya utepe mweupe nchini
wameeleza kusikitishwa na bajeti inayotengwa kutowekezwa kwenye vituo vya afya
hali inayopelekea ongezeko la vifo vya kina mama wajawazito na watoto kutokana
na huduma mbovu na kutoa wito kwa serikali kuona namna ya kuongeza bajeti na
kufuatilia kama zinatumika kwa lengo lililowekwa.
0 comments:
Post a Comment