Kenya imethibitisha visa viwili vya ugonjwa wa homa ya
manjano vilivyopatikana kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miongo miwili.
Visa vyote viwili vilitoka nchini Angola ambapo mripuko wa
ugonjwa huo umewauwa watu 150.
Kulingana na mwandishi wa BBC, Wakenya hao 2 waliwasili na
ugonjwa huo kutoka Angola ambapo wamekuwa wakiishi na kufanya kazi kwa zaidi ya
miaka 10.
Mgonjwa wa kwanza alifariki siku ya Jumatano katika
hospitali ya Kenyatta huku mgonjwa wa pili akiendelea kupata matibabu katika
hospitali hiyo.
Maafisa wa afya wanasema wameimarisha doria yao huku
wakiwahakikishia Wakenya kwamba hakuna hatari ya maambukizi ya moja kwa moja
kupitia mbu.
Homa ya manjano ilikuwa imeangamizwa nchini Kenya.
Haina dawa,lakini ishara zake zinaweza kukabiliwa.
Angola inapambana na mripuko wa homa hiyo na imeanza kutoa
chanjo kwa raia wake inayolenga watu milioni 7 katika eneo la Luanda
lililoathirika.
0 comments:
Post a Comment