Ndugu zangu,
Mtakumbuka kwamba mnamo tarehe 13 Oktoba 2015,
nilitangaza kuihama CCM na kurejesha kadi yangu ya uanachama kwenye ofisi ya
CCM Kata ya Mikocheni.
Nilitoa maelezo kwanini niliamua kujiondoa CCM (maelezo
hayo pia niliyabandika katika ukurasa wangu wa facebook).
Nilieleza kwamba CCM
imepoteza mwelekeo kwa kuamua kumnyima haki ya kugombea mcha mungu Edwad
Lowasa. Nikasema Edwad Lowasa ndiye chaguo la wana-CCM na ndiye chaguo la
Watanzania.
Nikasema nitakuwa mnafiki nikiendelea kubaki CCM huku naamini Edwad
Lowasa anafaa kuwa Rais kuliko John Pombe Magufuli.
Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka
niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowasa, nililewa ahadi ya Lowasa
kunipa uwaziri wa mambo ya Nje.
Niliamini mafuriko ya Lowasa ambayo yakanifanya
niamini kabisa anachukua nchi.
Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za
mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini
baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.
Leo natangaza kurudi CCM kwasababu nimeona kazi
nzuri ya Magufuli. Nimefanya kosa kubwa katika siasa ambalo nawasihi vijana
kwenye siasa wasifanye.
Nilihama kwa kwasababu ya mtu (Lowassa). Nimerudi
kwasababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba CCM ikiweka mtu hovyo
baada ya Magufuli, sitahama. Usemi wa CCM kwamba Chama Kwanza, Mtu Baadaye sasa
ndio nauona maana yake.
Niliwalaumu CCM kwa kumuacha Lowassa lakini sikujua
kwamba CCM ina uwezo wa miujiza wa kuibua jembe bora linaloitwa Magufuli.
Naomba mnisamehe kwa kulifanya jambo langu la
kujitoa CCM na kurudi CCM kuwa jambo la kitaifa ukizingatia kwamba sikuwa na
nafasi yoyote ya uongozi wa CCM wakati nahama na pia sijawahi kuwa hata Mjumbe
wa NEC ya CCM na nilikuwa nje ya ulingo wa siasa za CCM kwa miaka 20. Niliamua
kulifanya jambo kubwa ili kumsaidia Lowassa.
Na sasa nimeamua kulifanya jambo
kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za
washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia
swahiba wangu.
Naomba radhi kwa familia ya baba wa taifa mwalim
Nyerere kwa kuitumia kisiasa siku aliyokufa (tar 14 Octoba) na kutumia msiba
wake kutoa kauli za kisiasa zidi ya chama chake alichokiunda na ambacho hadi
anakufa alikuwa mwanachama.
Wananchi wote tumuombee Magufuli na tumsaidie kwani
tumepata nyerere mpya.
0 comments:
Post a Comment