Serikali wilayani Kasulu kupitia kamati ya ulinzi na
usalama ya wilaya hiyo imewasimamisha kazi na kuwakamata maafisa watatu wa
wakala wa misitu Tanzania TFS katika wilaya hiyo kutokana na kubainika kufanya
udanganyifu katika uvunaji wa mazao ya misitu wilayani humo baada ya kukamata
zaidi ya mbao elfu moja zikiwa zimevunwa kinyume cha sheria.
Akizungumza baada ya ukaguzi wa ghfla uliofanywa
katika kijiji cha Mvugwe na kukamata mbao hizo, mwenyekiti wa kamati hiyo
ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Kasulu Gerald Guninita amewataja maafisa hao
kuwa ni meneja wa wakala wa misitu wilaya ya Kasulu Donald Slaa na wafanyakazi
wawili wa TFS William Skoi na Jonathan Kaiza ambao wamebainika kuhalalisha kwa
kugonga muhuri wa serikali kwenye baadhi ya mbao nyumbani kwa mfanyabishara
badala ya kufanya kazi hiyo porini na kwamba maafisa hao wamekuwa tatizo badala
ya kuwa suluhisho la kulinda misitu katika wilaya hiyo.
Kwa upande wao wafanyabishara wa mbao katika
kijiji cha Mvugwe wilayani Kasulu,wamelalamikia hatua ya serikali kukamata mbao
zao, kwa kuwa wao wana vibali vyote vinavyowawezesha kuvuna mbao na
kusafirisha.


0 comments:
Post a Comment