Mwanamke mmoja alisafiri kwa ndege kutoka Istanbul
nchini Uturuki hadi mjini Paris akiwa na mtoto aliyemficha katika begi lake la
mkononi,shirika la ndege la Air Ufaransa limesema.
Shirika hilo limesema kuwa mtoto huyo aliyesafiri
bila kulipa nauli alipatikana ndani ya ndege hiyo siku ya Jumatatu usiku.
Duru katika shirika hilo iliambia shirika la habari
la AFP kwamba mwanamke huyo ni mkaazi wa Ufaransa ambaye alikuwa katika
harakati za kumfanya mtoto huyo kutoka Haiti kuwa wake.
Shirika hilo la ndege lilielezea mamlaka ya Ufaransa
lakini waendesha mashtaka wakaamua kutofungua mashtaka.
Mwanamke huyo alikuwa akingoja kuchukua ndege
nyengine mjini Istanbul lakini akazuiliwa kupanda ndege hiyo na mtoto huyo
,duru hiyo iliarifu AFP.
Alinunua tiketi nyengine na kumficha mtoto huyo
ndani ya begi.
Alipokuwa ndani ya ndege hiyo ,alimuweka mtoto huyo
katika miguu na kujifunika na blanketi ,lakini mtoto huyo wa kike alitaka
kwenda chooni na alionekana na abiria wengine.
Haijulikani mtoto huyo alikuwa na miaka mingapi
,duru moja ilieleza kwamba alikuwa na miaka minne huku nyengine ikisema alikuwa
na mwka mmoja ama miwili.


0 comments:
Post a Comment