Serikli imewasimamisha kazi watumishi sita wa sekta
ya mistu akiwemo meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini wa wakala wa huduma za
misitu nchini TFS na mshauri wa maliasili wa mkoa wa Rukwa kwa tuhuma za
kuzembea usimamizi wa misitu na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya
shilingi bilioni 500.
Hatua hiyo imechukuliwa na waziri wa maliasili na
utalii Profesa Jumanne Maghembe baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika
mistu ya hifadhi ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa na kukuta magogo mengi
yeneye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 500 yakiwemo yaliyokamatwa na
vyombo vya dola na mengine yakiwa bado msituni katika harakati za kuyasafirisha
kwenda nje ya nchi na ameagiza yakusanywe yote na serikali itafanya mchakato wa
kuyapiga mnada na fedha zitakazopatikana zitumike kwa manufaa ya uma.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kalambo Wilman Ndile
amesema kwa muda mrefu kumekuwa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu ambao
wamekuwa wakishirikiana na wahalifu kuvuna msitu katika wilaya hiyo kinyume cha
sheria na kuyapeleka upande wa Zambia kupata vibali bandia vinavyoonyesha kuwa
magogo hayo yamevunwa upande wa zambia hali ambayo imesababisha uharibifu
mkubwa wa misitu ya wilaya ya kalambo.
Nae mkurugenzi wa wakala wa huduma za misitu nchini TFS,Juma
Mgoo amesema serikali itaongeza nguvu katika kusimamia misitu ikiwemo kuajiri
watumishi wapya na walinzi wa misitu ili kuokoa rasilimali za taifa
zinazoteketea na kusababisha uharibifu mkubwa wa misitu ikiwemo ya vyanzo vya
maji.
Watumishi waliosimamishwa wametajwa kuwa ni pamoja
na meneja wa nyanda za juu kusini wa wakala wa huduma za misitu nchini tfs,
mshauri wa maliasili mkoa wa rukwa, na mameneja wa TFS wa wilaya za Kalambo na
sumbawanga pamoja na maafisa misitu wa halmashauri za wilaya za kalambo na
sumbawanga mkoani Rukwa.


0 comments:
Post a Comment