Watu wanne wamekufa papo hapo na wengine 26
wamejuriwa katika ajali ya gari iliyohusisha magari matatu iliyotokea
katika barabara ya mandela eneo la kwa Ali Hamza jiji Dar es Salaam.
Kamanda wa polisi kandaa maalumu ya Dar es
Salaam,Kamishna Simon Sirro amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 11
alfajiri ambao dereva lori ya mchanga lenye namba za usajili T44 DBH 7
likielekea Ubungo aliigonga nyuma daladala Toyota DCM yenye namba za usajili
T629 CRT na kusababisha ipoteze mwelekeo na kuhamia upande wa pili wa barabara
ambapo ikagongana na lori aina SCANIA yenye namba za usajili T109 DDX
lililokuwa limebeba Ngo'ombe na kusabaisha vifo vya abiria watatu na dereva wa
daladala hapohapo.
Kufuatia ajari hiyo baadhi ya majeruhi walikuwa
katika hali mbaya wameamishiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili,ambapo
akizunguza na waandishi wa habari afisa uhusiano wa Hospitali hiyo,Bi
Neema Mwangamo amekiri kupokea majeruhi watano ambao wako katika chumba cha
uangalizi maalum na wengine wameamishiwa katika taasisi ya tiba ya Mifupa-Moi-
kwa matibabu zaidi.
Aidha akizungumza na waandishi wa habari meneja
ustawi wa jamii na Mahusiano wa taasisi ya tiba mifupa-moi- Bwana Juma Almasi
amesema jumla ya majeruhi sita wamefikishwa katika taasisi hiyo kutoka
hopsitali ya taifa ya muhimbili idadi kubwa wakiwa wameumia katika sehemu za
miguu na vichwani na kuisisitiza wote wametambilika majina na maeneo
wanayoishi.
Idadi kubwa ya majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa
katika hospitali ya amana iliyopo manispaa ya ilala.



0 comments:
Post a Comment