Beki mkongwe wa real madrid Sergio Ramos amesema
mashabiki wa timu hiyo waliomzomea cristiano ronaldo kwenye mechi ya jana usiku
dhidi ya ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya as roma wanatakiwa kufikiri kwanza.
Ronaldo alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho
kwenye goli la pili la mchezo huo ambapo real ilishinda mabao 2 kwa bila na
kujihakikishia nafasi kwenye roo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya msimu huu.
Mreno huyo alizomewa na baadhi ya mashabiki wa real
madrid kwenye mechi hiyo kitenfo hicho kikihusishwa na kauli yake ya mwezi
febrauri kuwa wachezaji wenzake hawana uwezo kama wa kwake na ndo mana timu yao
lilifungwa na atletico madrid bao 1 kwa bila.
Sergio ramos ambaye ndo kapteni wa timu hiyo amesema
mashabiki wanatikuwa kufikiria kabla hawajamzomea mchezaji huyo kwani
anamchango mkubwa kwneye timu hiyo.
Kwa upande wake kocha wa real zinedine zidane
amesema walomzomea ronaldo wamemuongezea tu hamsa ya kufanya vyema kwenye
michezo inayofuata.
Nchini uingereza jinamizi la manchester united
limeanza kuiandama arsenal na kocha wake arsene wenger tayari ameshaanza
kuonesha wasiwasi wake kutokana na kuumia kwa wachezaji wake muhimu kwemye
mechi ya pili ya kombe la fa ambapo timu hiyo ilishinda mabao 4 kwa 0 dhidi ya
hul city.
Kiungo wa timu hiyo aaron ramsey alitolewa nje
dakika 16 baada ya kuingia kama mchezaji wa zida kwenye kipindi cha pili na
kuumia.
Walinzi per mertesacker and gabriel nao wameongeza
tatizo la majeruhi hasa upande wa mabeki huku laurent koscielny akiwa bado
hajapona.
Arsenal walishinda mechi hiyo ya pili ya mzunguko wa
5 wa fa cup na sasa watacheza robo fainali dhidi ya watford jumapili.
Na ushindi wa wikiendi hdidi ya warriros umeonekana
kuwatia nguvu los angeles lakers ambao alfajiri ya leo wamewafunga orlanod
magic kwa alama 107 kwa 98.
D'angelo russell aliendlea kuwafirahisha mashabiki
wa staples centre kwa namna alivyokuwa akicheza na kufanikiwa kutumbukiza alama
27.
Julius randle aliongeza vingine 23 huku jordan
clarkson akifunga 24 na kuwamaliza kabisa magic ambao alfajiri ya jana
walifungwa na warriors.
Mpaka mechi hiyo inaanza lakers bado walikuwa
wakishikilia rekodi ya timu mbovu ya pili kwenye msimu baada ya kufungwa mechi
51 wakishinda 14 tu.
Rekodi hiyo inashikiliwa na phoeniz suns.



0 comments:
Post a Comment