Kocha mkuu wa taifa Stars Charles Boniface Mkwassa
amejitolea kushirikiana na benchi la ufundi la timu ya taifa ya wanawake Twiga
Stars kukiandaa kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya
Zimbabwe wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Afrika ambazo zimepangwa
kufanyika nchini CAMEROON mwishoni mwa mwaka huu.
Mkwassa ambaye kabla ya kupewa kibarua cha kukinoa
kikosi cha taifa Stars aliwahi kuwa kocha mwenye mafanikio wa Twiga Stars
ambaye aliiwezesha timu hiyo kufuzu kwa fainali za Afrika za wanawake mwaka
2010 zilizofanyika nchini afrika kusini amesema alikwepo uwanjani wakati Twiga
Stars ilipochezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Zimbabwe mwishoni mwa wiki
iliyopita na kubaini mapungufu ambayo ameona anaweza kusaidia kuelekea mchezo
wa marudiano.
Kocha huyo maarufu kwa jina la 'MASTER' kutokana na
umahiri aliokua nao wa kusakata kandanda enzi zake amesema ameguswa na matokeo
waliyopata twiga Stars hivyo amejitolea kushirikiana na benchi la ufundi la
timu hiyo chini ya kocha nasra juma kuangalia makosa ya kiufundi na
kuyarekebisha kabla ya kukwea pipa kwenda zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa
marudiano.


0 comments:
Post a Comment