RAIS John Magufuli amewawataka Wakuu wa Mikoa nchini
kukamata watendaji wa kata wanaowavuruga wananchi na kuwaweka ndani ili kuwatia
adabu.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akiwaapisha viongozi
hao Ikulu jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku mbili baada ya kuwateua.
“Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka ndani hata masaa 48, wawekeni ndani ili wajue mnatakiwa kuheshimiwa,”amesema Rais Magufuli.
Hata hivyo, ameonesha kukerwa na tabia ya vijana
kutofanya kazi na badala yake kuwa mitaani wakicheza na kwamba, wakuu hao wa
mikoa wasimamie hilo.
“Kwa kweli ni aibu kuona kijana saa mbili au tatu asubuhi anacheza PoolTable halafu wazee wanalima, kamata peleka kambini walime kwa nguvu,” amesema.
Pia Rais Magufuli amewataka kuwaondoa wafanyakazi
hewa kwenye halmashauri zote nchini.
“Mmekula kiapo rasmi nawapa siku 15 kuanzia sasa kuhakikisha wafanyakazi hewa wanaondolewa serikalini mara moja.”


0 comments:
Post a Comment