Image
Image

Rais Magufuli awapa siku 15 wa kuu wa Mikoa kuondoa wafanyakazi hewa Makazini.




Saidi Msangi,Dar es Salaam.
Rais John Pombe Magufuli amewaapisha wakuu wa mikoa 25 na kuwapa siku 15 kuhakikisha kuwa wafanyakazi hewa wanaondolewa mara moja Makazini.
Dkt Magufuli amesema sababu za kufanya hivyo ni kuondoa majina yote ya wafanyakazi ambao ni hewa ambao wanalipwa fedha kila mwezi wakati kazi hawafanyi na hawapo katika maeneo yao ya kazi.
''Mwezi uliopita tulilipa mishahara ya wafanyakazi bilioni 500 mpaka 550 tukalipa na madeni ya nje bilioni 800 ,katika malipo ya wafanyakazi wengi ni mishahara hewa na serikali inalipa''. ''Sasa kuanzia leo wakurugenzi wote wapitie majina ya wafanyakazi na ambao hawapo kazini wayaondoe majina hayo haraka iwezekanavyo na wakurugenzi ambao hawatafanya hivyo ndani ya siku 15 watafukuzwa kazi na kupelekwa mahakamani''
Hata hivyo Rais Dkt Magufuli amewataka wakuu wa mikoa kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuwa tayari wamesaini kiapo cha kutumikia wananchi kwa uadilifu, weledi na kuzingatia sheria na taratibu za utumishi wa umma.
Katika hotuba yake fupi wakati akiwaapisha wakuu wa Mikoa Rais Magufuli pia ametaka viongozi wa maeneo husika kuhakikisha kuwa vijana wanafanya kazi kwa bidii kwani ndio nguvu kazi ya taifa.
Amesema kwamba ni jambo la aibuu kumkuta kijana asubuhi na mapema hafanyi kazi anakuwa mtaani akicheza Pool Table huku kina Mama na Wazee wakiwa wanalima mashambani na kuamuru viongozi wa maeneo husika kuwakamata na kuwapeleka makambini wakalime kwa nguvu.
"Nimeamua kuwateua wakuu wa mikoa nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika mikoa yenu, Napenda niwape pole kwa sababu mtakwenda kufanya kazi kweli kweli kutatua kero za wananchi wetu. Lakini pia niwaombe wakuu wa mikoa mkasimamie watu wafanye kazi hasa vijana haiwezekani vijana leo hii unamkuta saa mbili asubuhi anacheza Pool table wakati wa kina mama wanalima shambani, kama hawataki kufanya kazi kwa kupenda walazimishwe kufanya kazi.
" Amsema hii ni serikali ya Kazi tu hivyo kila mmoja anayo sababu ya kuheshimu muhimili wa dola kwa kuendana na kasi ya kazi tu ili kusudi kufika pale tunapo pataka huku akisema kwa Tanzania tupo nyuma hivyo hapendi kuona halii hii ikiendelea kwani ni jambo la aibu.
 Wakati wa Maagizo yake kwa wakuu wa mikoa amewaeleza kuwa katika mikoa wanayoenda wahakikishe kwamba suala la wananchi kufanya kazi zao kwa amani na utulivu linakuwapo kwa asilimia miamoja na kuwataka kuhakikisha wanapambana kutokomeza makundi ya majambazi kusudi wananchi wanapoenda sehemu moja ama nyingine kusiwe na msaada wa polisi kwa kuwa nchi yetu ni ya amani na utulivu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment