Msongamano mkubwa wa wagonjwa katika Hospitali ya rufaa
ya KCMC umesababisha madaktari kutoa huduma katika mazingira magumu na hatari kwao wenyewe na pia kwa
wagonjwa na serikali imeombwa kuongeza
jitihada za kuboresha hospitali za mikoa
na wilaya ili kupunguza tatizo hilo .
Idadi
kubwa ya wagonjwa wameonekana wakiwa wamelazwa nje
ya wodi na kwenye
njia za kuingia
wodini hali ambayo mkurugenzi mtendaji wa Hosipitali
hiyo amesema wanaendelea kuikabili
kwa kuongeza majengo
likiwemo la tiba ya moyo linalojengwa
kwa ufadhili wa Mwenyekiti
mtendaji wa makampuni
ya IPP Dr.Regnald Mengi.
Hata hivyo
baadhi ya wagonjwa
wamesema licha ya kulazwa
knje ya wodi meendelea
kuhudumiwa na wameandikiwa kuja
katika hosipitali hiyo kutokana
na ukosefu wa
huduma bora , madaktari wenye
sifa na vitendea kazi katika
hosipitali za miko , wilaya na
vituo vya afya.
Baadhi ya
wasimamizi na wadhamini
wa hosipitali hiyo iliyoanzishwa miaka
45 iliyopita ikiendeshwa
kwa ushirikiano wa
serikali na kanisa
la kkkt ambayo
inahudumia wagonjwa kati
ya 600 na
800 kwa siku
ikiwa na vitanda
600 wamewataka watendaji
kuongeza uwajibikaji ili
kukidhi matarajio ya
wogonjwa na kuendelea
kuwapa moyo na
imani.
Kcmc ni
miongoni mwa hosipitali nne
kubwa za rufaa
hapa nchini ambazo
zimekuwa kimbilio la wananchi
wenye magonjwa yaliyoshindikana maeneo
mengine,nyingine ikiwa ni
muhimbili , iliyoko daressalam ,
bugando ya mwanza na hosipitali ya rufaa
ya mbyeya.


0 comments:
Post a Comment